Imam Hussein (a.s) ni lazima abaki kuwa bendera ya haki milele.Na bendera ya Haki haiwezi kusimama upande wa batili (uovu), wala haiwezi kuchukua rangi ya batili.
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- “Harakati ya Imam Hussein (a.s) ilikuwa ni harakati ya heshima na utukufu - Heshima ya Haki, Heshima ya Dini, Heshima ya Uongozi wa Kiislamu (Al_Imamah), na Heshima ya njia ile ile aliyokuja nayo Mtume wa Uislamu, Muhammad (s.a.w.w).”
Kiongozi wa Mapinduzi ameongeza:
Imam Hussein (a.s) ni lazima abaki kuwa bendera ya haki milele.
Na bendera ya Haki haiwezi kusimama upande wa batili (uovu), wala haiwezi kuchukua rangi ya batili.
Imam Hussein (a.s) alitangaza kwa msimamo wa wazi akisema:
"هیهات منّا الذّلّة"
“Kamwe hatutakubali udhalili (udhalilishaji)”
Hapo chini , tumekuwekea baadhi ya Picha za Leo za Maombolezo ya Tasu'a - Katika Mkoa wa Tabriz - Iran
Your Comment