A'shura ni Tukio Kubwa la kihistoria ambalo kamwe haliwezi kusahaulika katika kurasa za Kihistoria kutokana na Mauaji makubwa yaliyotenswa na Muovu Yazid bin Muawia Siku hiyo, kwa kuchinja Mjukuu wa Mtume Muhammad (saww) - Al-Imam Al-Hussein (as) na Masahaba wake katika Ardhi ya Karbala. Damu yake ilimwagwa kwa dhulma Ardhini na Siku ya Kiyama watajua ni mgeuko gani wanaogeuka madhalimu hao.
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Leo hii Tarehe: 10 Muharram, 1447H, Sawa na Tarehe 6 Julia, 2025, Waislamu wafuasi na Wapenzi wa Ahlul-Bayt (as) wameadhimisha Tukio la Shahada ya Imam Hussein (as) katika Ardhi ya Karbala, lililofanyika Siku ya 10 (A'shura) ya Mwezi wa Muharram, mwaka 61 Hijria baada ya Yazid bin Muawia kuamuru majeshi yake kufanya Mauaji makubwa dhidi ya Imam Hussein (as) na Masahaba wake na familia ya Mtume Muhammad (saww) kwa ujumla. Ni Tukio chungu mno ambalo kamwe haliwezi kusahaulika kwa Waumini wa Umma huu wa Kiislamu, bali kwa Wanadamu wote huru wenye Utu na ubinadamu.
Waumini mbalimbali wamehudhuria katika Maandamano ya amani ya kulaani Mauaji ya halaiki ya Karbala dhidi ya Familia ya Mtume Muhammad (saww) na Masahaba wote Mashahidi wa Karbala. Maandamano hayo yameanzia Ilala Boma Jijini Dar-es-salaam na kuishia katika Uwanja wa Pipo - Kigogo Post.
Miongoni mwa walio hudhuria katika Masira haya ni Hojjatul-Islam Wal Muslimin, Dr. Ali Taqavi, Rais wa Jamiat Al-Mustafa (s) - Dar-es-salaam - Tanzania.
Masheikh mbalimbali na Walimu wa Jamiat Al-Mustafa (s) - Dar-es-salaam.
Waumini na Wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya Kidini.
Mbunge wa Kinondoni, Mheshimiwa Abbas Talimba.
Na Waumini mbalimbali wa Mkoa wa Dar-es-salaam na nje ya Dar-es-salaam.
Tumekuwekea hapo chini picha zaidi za Masira haya ya Maombolezo ya A'shura.
Mwenyezi Mungu akulipeni ujira mkubwa Duniani na Akhera na mzidi kushikamana na Njia ya Haki, ukweli na uadilifu, na hakika hiyo ndio Njia ya Mtume wetu Muhammad (saww) na Ahlul-Bayt wake Watoharifu.
Your Comment