Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Viongozi mbalimbali wa Taasisi mbalimbali za Kiislamu na Kiserikali wamehudhuria katika Maandamano ya Amani ya Maombolezo ya A'shura Nchini Tanzania, ambayo yamefanyika kwa mafanikio makubwa katika mwaka huu wa 1447 Hijria wa Maombolezo ya Muharram. Masira haya yamefanyika katika Mitaa ya Posta Jijini Dar-es-salaam - Tanzania, yakihudhuriwa na Viongozi hao ambao ni pamoja na: Hojjat al-Islam wal-Muslimin, Dr. Ali Taqavi - Rais wa Jamiat Al-Mustafa (s), Tanzania. Wengine ni Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Naibu spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mussa Azan Zungu na Viongozi wengine wa Kiserikali na Kiroho.
6 Julai 2025 - 17:19
News ID: 1705049
Tizama Picha zaidi hapo chini
Your Comment