Mwaka huu wa 1447H, Masira au Matembezi ya amani ya Ashura katika kuyaenzi Mapinduzi ya Haki ya Imam Hussein (as) na kuhuisha mnasaba wa shahda yake katika ardhi ya Karbala, yametia fora baada ya waumini wengi kujitokeza kwa wingi nchni Tanzania kwa ajili ya kushiriki katika masira hiyo na kuufikishia ulimwengu ujumbe maridhawa kuwa dunia baada ya Ashura ilitambua na inaendelea kutambua kuwa Uislamu ni Dini iliyo hai na itabakia kuwa hai, hata kama waovu watajitahidi kuizima mithili ya muovu Yazid bin Muawia, lakini hawatafanikiwa kamwe kama alivyofeli muovu huyo katika vita vya Karbala na Bani Umaiyya kwa ujumla.
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Waislamu wapenzi na wafuasi wa Imam Hussein (as) na Ahlu Bayt Rasulillah (s.a.w.w) kwa ujumla, wanazidi kuongezeka duniani kote katika mwelekeo wa kuhuisha ujumbe wa Karbala uliotolewa na Imam Hussein (as) katika harakati yake ya Mapinduzi ya Kiislamu dhidi ya udhalimu na madhalimu, dhidi ya uovu na waovu, na iliyokuwa kwa ajili kutetea na kueneza haki, ukweli na uadilifu duniani. Harakati hiyo imekuwa ni ishara ya ujasiri na ushujaa katika kuitetea haki na uadilifu na kuhuisha na kudumisha maadili safi ya kiislamu kwa walimwengu wote.
Mwaka huu wa 1447H, Masira au Matembezi ya amani ya Ashura katika kuyaenzi Mapinduzi ya Haki ya Imam Hussein (as) na kuhuisha mnasaba wa shahda yake katika ardhi ya Karbala, yametia fora baada ya waumini wengi kujitokeza kwa wingi nchni Tanzania kwa ajili ya kushiriki katika masira hiyo na kuufikishia ulimwengu ujumbe maridhawa kuwa dunia baada ya Ashura ilitambua na inaendelea kutambua kuwa Uislamu ni Dini iliyo hai na itabakia kuwa hai, hata kama waovu watajitahidi kuizima mithili ya muovu Yazid bin Muawia, lakini hawatafanikiwa kamwe kama alivyofeli muovu huyo katika vita vya Karbala na Bani Umaiyya kwa ujumla.
Leo hii, kupitia harakati ya Imam Hussein (as), Dunia imewatambua waovu na matwaghuti ambao ndio kambi ya Yazid bin Muawia, na pia imewatambua watu wema wenye kumuabudu Allah (swt) na kuwafuata Ahlul-Bayt (as), ambao ndio kambi ya wafuasi wa Mtume Muhammad (saww) na Aali zake watoharifu (as).
Your Comment