Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania tumekuwa na Ushirikiano mzuri wa kujenga 'Mahusiano Mazuri' kati ya Waislamu na Wakristo na Viongozi wa Mila mbalimbali.
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania, Askofu Dkt. Gabriel Ole Maasa, amebainisha Malengo ya Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania katika kusajiriwa kwake kuwa ni: Ili kushiriki katika jitihada za Serikali za kudumisha Amani na Utulivu uliopo Nchini.
Jambo hili, Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania inalifanyia kazi katika Mikoa mbalimbali Nchini na imefika ndani zaidi katika Kata mbalimbali bali kila kona ya nchi, katika kudumisha Amani na Utulivu nchi yetu.
Aliendelea kubainisha akisema: Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania tumekuwa na Ushirikiano Mzuri wa kujenga Mahusiano mazuri kati ya Waislamu na Wakristo na Viongozi wa Mila mbalimbali.
Tunahakikisha kwamba: Hakuna Muislamu au Mkristo atakayetumia Lugha ya Dini yake kuvuruga Amani, au mtu kutumia utaratibu wa Mila na Desturi yake kuvuruga Amani.
Tunahakikisha watu hawa Watatu, wanaweza kuishi kwa pamoja kwa 'Raha na Amani' katika nchi yao ambayo Mungu amewapatia.
Jumuiya yetu ya Maridhiano na Amani ina uhusiano Mzuri na Serikali, na walezi wake ni pamoja na Viongozi wastaafu wa Serikali. Mbali na hilo, katika Mikoa mingi Nchini, walezi wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani ni Wakuu wa Mikoa, na Wakuu wa Wilaya. Lengo ni kuwaunganisha Watanzania wote waendelee kuishi katika nchi yao nzuri na ya Amani waliyopewa na Mwenyezi Mungu.
Idara za Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania:
Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania, katika utendaji kazi wake, inazo idara 15 kwa sasa.
Miongoni mwa idara hizo, ni pamoja na idara ya mipango, uchumi na fedha.
Hii ni katika kuhakikisha kwamba chombo chetu kinatenda kwa mipango sahihi na ya Kitaalamu inayokubalika.
Tunayo idara ya utalii na Utamaduni. Na hili linaonyesha kwamba Watanzania tunaweza kuhamasishana kuendeleza utalii wetu wa ndani.
Tunayo idara ya Dini, inayojumuisha Waislamu, Wakristo na Viongozi wa Mila. Linapotokea Jambo lolote la Kidini au kimila, idara hiyo inahusika.
Idara zingine ni pamoja na idara ya Vijana, idara ya Wanawake, idara ya utatuzi wa migogoro, idara ya kamati ya maadili, idara ya michezo, idara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, idara ya Habari na mawasiliano, idara ya uhamasishaji na uwajibikaji, zote hizo hizo ni idara za Jumuiya ya Maridhiano na Amani ambapo hilo linaonyesha kuwa chombo hiki kinafanya kazi zake Kisasa zaidi katika kukidhihi malengo na mahitaji ya Watanzania wanaoishi leo hii katika nchi yao ndani ya mwaka wa 2025.
Changamoto:
Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania - tumekuwa na Changamoto Moto kadhaa ambazo tungefurahi zikipatiwa ufumbuzi na utatuzi. Hususan Changamoto ya kutokuwa na Ofisi za Jumuiya katika Mikoa na Wilaya mbalimbali.
Viongozi wetu wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania hawana Ofisi katika maeneo hayo.
Tunaomba Ushirikiano wa karibu ili wenyeviti wetu wa Mikoa na Wilaya au Viongozi wa Jumuiya yetu Mikoani na Wilayani waweze kupata Ofisi kwa ajili ya kufanya Kazi yao kwa Utulivu, kwa Amani na kwa Ufanisi zaidi. Wamekuwa wakifanya Vikao vikao kwa kukutana ima hotelini au maeneo yasiyo rasmi na kwa tabu zaidi.
Tunaomba Mheshimiwa, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, utasaidie katika ufumbuzi wa changamoto hii.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania, Dkt.Gabriel Ole Maasa akifafanua na kuchambua Malengo ya Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania mbele ya Mgeni Rasmi na Mlezi wa JMAT-TAIFA - Nabii Mkuu Dkt. Geordavie na Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, pamoja na Viongozi mbalimbali wa JMAT akiwemo Mwenyekiti wa JMAT-TAIFA Sheikh Dkt. Alhad Mussa Salum.
Mipango ya Jumuiya ya JMAT-TAIFA:
Mipango na Fikra ya Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania kwa sasa ni kujenga Ofisi zetu wenyewe na jengo la Makao Makuu ya Jumuiya na Kumbi za Mikutano yetu na shughuli zetu.
Maeneo ambayo tunalenga kujenga Ofisi zetu na Ofisi ya Makao Makuu ya Jumuiya yetu, ni pamoja na Mkoa wa Dodoma, ambao ndio Makao Makuu ya nchi yetu. Mkoa huu ni Mkoa Mzuri, unaong'ra na kukua kwa Kasi kubwa.
Ombi letu kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, tunaomba tusaidiwe kupata eneo ambalo litatutosha kwa ajili ya kujenga kumbi zetu za kutosha, na Ofisi zetu za kutosha.
Tukipata eneo Dodoma kwa msaada wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, tunaamini kuwa suala la kuanza ujenzi wa Kumbi za Mikutano na Ofisi zetu ni dogo sana, kwa sababu tunaye mlezi wetu Nabii Mkuu Dkt. Geordavie ambaye ndiye Mgeni wetu Rasmi (katika Mkutano huu wa Viongozi) kwake hili ni suala rahisi mno, kwa maana ujenzi utaanza kwa haraka sana.
Wameshimiwa Viongozi, naomba kuwasilisha, na Mungu awabariki sana.
Askofu Dkt. Gabriel Ole Maasa - Katibu Mkuu JMAT-TAIFA.
Dodoma - Tanzania.
Your Comment