Sunna ya Mtume Muhammad (s.a.w.w), na ina nafasi kubwa katika kulinda maadili, kuleta utulivu wa nafsi, kuimarisha imani na kudumisha usalama wa kijamii.
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Leo hii, Ijumaa 11, Julai, 2025, Swala ya Ijumaa imeongozwa na Sheikh Mohammed Mwazoa katika Kituo cha Taasisi ya Kimataifa ya Al-Mustafa (s), Dar-es-salaam - Tanzania.
Mada ya Khutba: Faida za Ndoa Katika Jamii
Katika khutba yake, Sheikh Mwazoa alizungumzia umuhimu wa ndoa katika maisha ya mtu binafsi na jamii kwa ujumla.
Alisisitiza kuwa ndoa ni Sunna ya Mtume Muhammad (s.a.w.w), na ina nafasi kubwa katika kulinda maadili, kuleta utulivu wa nafsi, kuimarisha imani na kudumisha usalama wa kijamii.
Aliongeza kuwa ndoa huzuia mmomonyoko wa maadili na huchangia katika kulea kizazi kilicho bora.
Pia aliwahimiza Waumini kurahisisha suala la ndoa kwa vijana na kuzingatia misingi ya Kiislamu katika uanzishaji wa familia.
Katika hitimisho, Sheikh aliwaasa Waumini kuifanya ndoa kuwa njia ya kumridhisha Mwenyezi Mungu na kuleta baraka katika jamii.
Your Comment