Umoja wa Umma wa Kiislamu na Mshikamano wa Kimataifa dhidi ya dhulma, huku akisisitiza kuwa umoja na mshikamano kati ya Waislamu ni silaha madhubuti ya kulinda heshima ya Umma wa Kiislamu.
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Jijini Nairobi, Dkt. Ali Gholampour, leo amehudhuria Swala ya Ijumaa katika Msikiti wa Makina uliopo Kibra, Nairobi.
Katika tukio hilo, Dkt. Gholampour alipata fursa ya kuzungumza na jamii ya Kiislamu, ambapo alitoa hotuba kuhusu umuhimu wa Umoja wa Waislamu.
Aidha, alieleza kwa kifupi kuhusu matukio ya hivi karibuni katika eneo la Mashariki ya Kati, ambapo nchi yake ilishambuliwa lakini ilijitetea kwa ujasiri mkubwa.
Hotuba yake ilisisitiza Umoja wa Umma wa Kiislamu na Mshikamano wa Kimataifa dhidi ya dhulma, huku akisisitiza kuwa umoja na mshikamano kati ya Waislamu ni silaha madhubuti ya kulinda heshima ya Umma wa Kiislamu na amani ya jamii ya Kiislamu.
Your Comment