Katika mtazamo wa Kiislamu, michezo ni njia halali ya kuimarisha mwili na kuendeleza undugu. Mtume Muhammad (s.a.w.w) alihimiza mazoezi ya mwili kama vile kurusha mishale, kupanda farasi, na kuogelea - ikiashiria kuwa afya bora ni sehemu ya maisha ya Kiislamu.

12 Julai 2025 - 17:24

Afya Bora ni Sehemu ya Maisha ya Kiislamu - Michezo ni Afya | Ushindi wa Kifahari kwa Wahitimu wa Al-Hadi: 5–1 Dhidi ya Wanafunzi wa Sasa +Picha

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Katika pambano la kusisimua la mpira wa miguu lililowakutanisha Wanafunzi wa zamani na wale wa sasa wa Kituo cha Kiislamu cha Al-Hadi(as), timu ya wahitimu iliibuka kidedea kwa ushindi wa mabao 5 kwa 1.

Mechi hiyo haikukosa msisimko, kwani iliakisi mchuano wa uzoefu dhidi ya ari ya ujana. Kwa maana: Uzoefu umeshinda nguvu mpya na ari ya ujana.

Wahitimu walionyesha kujipanga kikamilifu na uratibu mzuri wa timu, wakimiliki mbinu makini, na uwezo wa kumalizia nafasi kwa ustadi mkubwa - na hayo ndio mambo yaliyopelekea wao kuibuka na ushindi wa kishindo.

Kwa upande wao, Wanafunzi wa sasa walionesha moyo wa kupambana na kutokata tamaa wakiwa na vipaji vinavyochipukia, hilo liliwasaidia kutoa changamoto kwa wapinzani wao kwa muda kadhaa, lakini hatimaye walilazimika kukubali uwezo wa waliowatangulia kiuzoefu katika masuala ya soka.

Mchezo huu, mbali na ushindani wake, ulikuwa pia ni fursa ya kuimarisha mshikamano, kukuza afya, na kuendeleza urafiki kati ya vizazi viwili vya taasisi hiyo tukufu (wahitimu na wanafunzi wa sasa).

Katika mtazamo wa Kiislamu, michezo ni njia halali ya kuimarisha mwili na kuendeleza undugu. Mtume Muhammad (s.a.w.w) alihimiza mazoezi ya mwili kama vile kurusha mishale, kupanda farasi, na kuogelea - ikiashiria kuwa afya bora ni sehemu ya maisha ya Kiislamu.

Kwa hivyo, michezo kama hii si burudani tu, bali pia ni utekelezaji wa maadili ya dini kuhusiana na: Kujenga mwili, kukuza ushirikiano, na kushirikiana kwa njia ya heshima.

Your Comment

You are replying to: .
captcha