Sambamba na Programu hiyo, ilisomwa Surat al-Fatiha moja na Surat Al- Ikhlasi mara tatu kwa ajili ya kuwarehemu Marhumina wa Kiislamu.
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Taasisi ya Hujjatul - Asr Society Of Tanzania, imefanya
Majilis ya Maombolezo ya baada ya Mauaji ya A'shura katika Mwezi wa Muharram, katika eneo Utete Rufiji, Masjid Imam Baqir (as), ambapo zilikusanyika katika Masjid hiyo Madrasa kadhaa ambazo ni: Madrasa ya Imam Baqir (as), Madrasa ya Imam Jawaad (as), na Madrasa ya Imam Mahdi (a.t.f.s).
Samahat Sayyid Arif Naqvi alitoa Mawaidha na Nasaha kwa Waumini na kuwaasa kuendelea kumuezi Imam Hussein (as) kupitia kuitafuta Elimu ya Dini Tukufu ya Kiislamu, kueneza Elimu hiyo, na kuipigania Dini Tukufu ya Kiislamu kwa Hali na Mali.
Sambamba na Programu hiyo, ilisomwa Surat al-Fatiha moja na Surat Al- Ikhlasi mara tatu kwa ajili ya kuwarehemu Marhumina wa Kiislamu.
Your Comment