Darsa hili, limeongeza ari ya kielimu na kimaanawi kwa wanafunzi wa Hawza ya Imam Zainul-Abidina (as).
Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Leo Alhamisi, tarehe: 17/7/2025 Programu ya Asubuhi ya Kiroho - imefanyika katika Hawza ya Imam Zainul Abidin (a.s) - Burundi, na Mada iliyowasilishwa ilihusiana na: Njia za Mafanikio kwa Wanafunzi wa Dini.
Mtoa mada: Sheikh Ismail - kutoka nchini Tanzania.
Katika Darsa hili la Kiroho, lililofanyika katika siku hizi za Mwezi wa Muharram, mgeni katika Hawza hiyo, ambaye ni Sheikh Ismail kutoka nchini Tanzania alitoa mawaidha yenye manufaa juu ya mbinu na njia za kufanikisha masomo na maisha ya Wanafunzi wa Elimu ya Dini.
Mambo muhimu aliyoyasisitiza ni pamoja na:
1. Ikhlasi katika nia:
Kusoma kwa ajili ya radhi za Mwenyezi Mungu na kuhudumia jamii.
2. Mpangilio mzuri wa muda:
Kugawa muda kwa ajili ya kusoma, ibada, na kupumzika.
3. Kujiepusha na uvivu na uzembe:
Kuvumilia matatizo na kujitahidi katika njia ya elimu.
4. Kushirikiana na walimu na kunufaika na tajriba zao.
5. Kujikurubisha kwa Ahlulbayt (as):
Haswa kuchukua funzo kutoka kwa Imam Husayn (a.s) katika mwezi huu wa Muharram.
Programu ilianza kwa usomaji wa Qur'an Tukufu, na ikahitimishwa kwa mawaidha ya kiroho yaliyogusa nyoyo za Wanafunzi.
Tukio hili limeongeza ari ya kielimu na kimaanawi kwa Wanafunzi wa Hawza ya Imam Zainul-Abidina (as).
Your Comment