Katika Darasa hili, mbali na usomaji wa Aya Tukufu, masomo ya tafsiri ya Qur'an, maadili na malezi ya Kiislamu hutolewa kwa njia ya kufundisha na kuhamasisha. Na ushiriki katika madarasa haya ya Qur'an Tukufu uko wazi kwa wote, na ni fursa adhimu ya kukuza elimu na kuimarisha roho za washiriki.
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Leo, Alhamisi, Tarehe 17/07/2025, Darasa la Kila Wiki la Qur'an Tukufu kwa Wanafunzi Jamiat Al-Mustafa (s) - Dar-es-salaam - Tanzania limeendelea likiongozwa na kusimamiwa na: Sheikh Muhammad Jafari.
Wapenzi wa Qur'an Tukufu wanajulishwa kuwa darasa hili la kila wiki la usomaji na tafsiri ya Qur'an Tukufu, linafanyika pasina Mabadiliko yoyote katika kila siku ya Alhamisi. Kila mtu yuko kuja kushiriki na kufaidika na Darsa la usomaji na Tafsiri ya Qur'an.
Kawaida, Darasa hili huhudhuriwa na Wanafunzi na wapenda elimu ya Dini Tukufu ya Kiislamu, katika mazingira ya kiroho chini ya uongozi na Usimamizi wa Sheikh Muhammad Jafari.
Katika Darasa hili, mbali na usomaji wa Aya Tukufu, masomo ya tafsiri ya Qur'an, maadili na malezi ya Kiislamu hutolewa kwa njia ya kufundisha na kuhamasisha.
Kwa Mantiki hiyo, ushiriki katika madarasa haya uko wazi kwa wote, na ni fursa adhimu ya kukuza elimu na kuimarisha roho za washiriki.
Your Comment