Kikao hiki kililenga kusikiliza kwa karibu matatizo, maoni, na wasiwasi wa Wanafunzi, sambamba na kujadili mabadiliko yanayotarajiwa kuanza kutekelezwa kuanzia muhula ujao wa masomo.
Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) - ABNA- Kikao Maalum kimefanyika katika Chuo cha Kidini cha Jamiatul Mustafa (s) - Nchini Malawi kikimuhusisha mas-uli anayehusika na masuala ya kitamaduni na Wanafunzi wa Dini, na walijadiliana kuhusiana na changamoto mbalimbali zinazowakabili wanafunzi wa Chuo hicho na kuzitaftia ufumbuzi.
Kama tulivyoashiria, kikao hiki kililenga kusikiliza kwa karibu matatizo, maoni, na wasiwasi wa Wanafunzi, sambamba na kujadili mabadiliko yanayotarajiwa kuanza kutekelezwa kuanzia muhula ujao wa masomo.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa waandaaji wa kikao hicho, mabadiliko hayo yanakusudia kuboresha mazingira ya masomo na kuimarisha ufanisi wa kielimu na kitamaduni.
Your Comment