Hafla hiyo imeonesha uzito na heshima kubwa aliyonayo Samahat Sheikh Dr. Alhad Mussa Salum katika jamii ya Kiislamu na ya kitaifa kwa ujumla.
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Leo hii, Tarehe 20 Julai, Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mardhiano na Amani Tanzania (JMAT), Sheikh Dkt. Alhad Mussa Salum, ameongoza hafla kubwa ya kiheshima katika ukumbi wa DYCC Temeke kwa ajili ya "Walima" wa mwanae Islah, aliyehitimisha Ndoa yake wiki iliyopita nchini Kenya.
Hafla hii imepambwa kwa uwepo wa viongozi wa ngazi mbalimbali wakiwemo Masheikh wakubwa kutoka maeneo mbalimbali ya nchi, pamoja na wawakilishi wa dini nyingine, wote wakijumuika kwa utulivu na heshima kubwa kwa ajili kufurahia jambo Tukufu la Ndoa ya Mtoto wa Kiongozi wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania.
Mgeni Rasmi wa Hafla hii alikuwa ni: Mheshimiwa Mufti wa Tanzania, Dkt.Abubakar Zubair bin Ally akiambatana na timu kutoka Makao Makuu ya BAKWATA, wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Taasisi hiyo, ambao wote kwa pamoja wamehudhuria na kuipamba hafla hii ikiwa ni ishara muhimu ya mshikamano wa kidini na kijamii.
Shekh Muharramu Mwaita alitumia fursa aliyopewa kumpongeza Dkt. Alhad Mussa Salum kwa kuonesha Uongozi bora kwa kuzingatia nyakati za Sala katika ratiba za Hafla mbalimbali, hasa Sala ya Adhuhuri ambayo ilitekelezwa kwa nidhamu Sahihi katika Hafla hiyo, tofauti na baadhi ya hafla nyinginezo ambapo Sala huwa haizingatiwi wakati wake katika ratiba na hivyo kutokupewa kipaumbele kinyume na anavyotaka Mwenyezi Mungu.
Hafla hiyo imeonesha uzito na heshima kubwa aliyonayo Samahat Sheikh Dkt. Alhad Mussa Salum katika jamii ya Kiislamu na ya kitaifa kwa ujumla.
Tukio hili limeacha alama ya mshikamano, heshima na kielelezo cha uongozi wa kiroho wenye maadili.
Tumekuwekea hapo chini picha zaidi za tukio hili adhimu
Your Comment