Majalis hizi zinaendelea kuhuishwa kwa Heshima na Mapenzi makubwa kwa Ahlul Bayt (a.s), ambacho kwa hakika ndio Kizazi Bora cha Mtukufu Mtume wetu Muhammad (saww) alichotuachia tushikamane nacho na kukionyesha Mapenzi makubwa, na sio Mapenzi tu, bali ni Mawadda ambayo ni zaidi ya Mapenzi, na hii ni kwa mujibu wa Qur'an Tukufu. Na Sisi tunajifakharisha kwa kupata Taufiq ya kushikamana na Kizazi Kitukufu cha Mtume wetu Muhammad (saww) na kuwafuata wao katika mambo yote ya Dini Tukufu ya Kiislamu na ya Dunia yetu, na si vinginevyo.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Majlisi Tukufu ya kuadhimisha Shahada ya yule ajulikanae kama "Pambo la Wenye Kuabudu", Imam Ali - Zaynul Aabidin (a.s), Mjukuu wa Mtume (s.a.w.w) na Mwana wa Imam Hussein (a.s), Imam wa nne (4) katika mlolongo wa Maimamu wa Ahlul Bayt (a.s), imefanyika kwa Hamasa na kwa mahudhurio Maridhawa ya Wapenzi na Wafuasi wa Ahlul-Bayt (as) katika viunga vya Msikiti wa Mwanzaroad Mkoani Tabora.
Majlisi hii ya Maombolezo ya Shahada ya Imam Zainul-Abidina (as) iliambatana na:
1_Nauha na Maatam za Maombolezo.
2_Hotuba Maridhawa juu ya maisha ya Imam Zaynul Aabidina (as).
3_Dua na Munajat za Kiroho.
4_Swala ya Jamaa.
Majalis hizi zinaendelea kuhuishwa kwa Heshima na Mapenzi makubwa kwa Ahlul Bayt (a.s), ambacho kwa hakika ndio Kizazi Bora cha Mtukufu Mtume wetu Muhammad (saww) alichotuachia tushikamane nacho na kukionyesha Mapenzi makubwa, na sio Mapenzi tu, bali ni Mawadda ambayo ni zaidi ya Mapenzi, na hii ni kwa mujibu wa Qur'an Tukufu.
Na Sisi tunajifakharisha kwa kupata Taufiq ya kushikamana na Kizazi Kitukufu cha Mtume wetu Muhammad (saww) na kuwafuata wao katika mambo yote ya Dini Tukufu ya Kiislamu na ya Dunia yetu, na si vinginevyo.
Kwa hakika Imamu Zaynul Aabidina (a.s) alikuwa kielelezo cha subira, ibada na huruma.
Your Comment