Kitengo cha Tabligh Mkoani Kagera kinatoa rambirambi kwa Waislamu wote Duniani kwa msiba wa Karbala ambao vuguvugu lake ni la kudumu katika Nyoyo za Waumini hususan Wafuasi wa Ahlul-Bayt (as).

22 Julai 2025 - 14:30

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Majlisi ya Shahada ya Imam Hussein (a.s) na Matukio ya Baada ya Ashura, imefanyika  Kamachumu katika Kituo cha Wafuasi wa Ahlul-Bayt (as) Kinachoitwa: Kamachumu Shia Centre (Masjidu Nuruzerabai), Tarehe: 20 Julai, 2025, ambapo iliandaliwa na kusimamiwa na Taasisi ya: Murtaza Foundation

Majlisi ya Shahada ya Imam Hussein (a.s) na Matukio ya Baada ya Ashura, Kamachumu + Picha

Wazungumzaji katika Majlisi hiyo ni pamoja na: 

1_Sheikh Abdul-Malik Kawaya ambaye alisisitiza umuhimu wa ibada, kusoma Qur’an, na kushikamana na Watukufu wa Ahlul Bayt (a.s).

2_Sheikh Hussein Shahid Ntarugera ambaye alisoma Majlisi ya Shahada ya Imam Hussein (as) kwa hisia kubwa, na kuwagusa hadhira Kiroho.

3_Mwenyekiti wa Khoja Shia Ithna-Asheri Jamaat alitoa shukrani kwa waliohudhuria Majlisi hiyo na kuwahimiza kuwaombea Amani na Ushindi Waislamu na Wananchi wa Wapalestina kwa ujumla.

Majlisi ya Shahada ya Imam Hussein (a.s) na Matukio ya Baada ya Ashura, Kamachumu + Picha

Kitengo cha Tabligh Mkoani Kagera kinatoa rambirambi kwa Waislamu wote Duniani kwa msiba wa Karbala ambao vuguvugu lake ni la kudumu katika Nyoyo za Waumini hususan Wafuasi wa Ahlul-Bayt (as).

Ripoti hii imetolewa kwa hisani kubwa ya: 

Kitengo cha Tabligh - Bukoba, Murtaza Foundation.

Your Comment

You are replying to: .
captcha