"There are no more words to speak about what’s going on in Gaza" - (Hamna maneno mengine ya kusema kuhusu kilichoko - kinachoendelea- Gaza).

26 Julai 2025 - 23:22

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Katika mjadala wa Bunge la Ulaya mnamo Februari 27, 2024, mwanasiasa maarufu wa Uswidi, Mjumbe wa Bunge la Ulaya (MEP) Abir AlSahlani, alifanya maandamano ya ishara ya ukimya bungeni kuonyesha kukerwa kwake na ukimya wa sera za Ulaya mbele ya mauaji yanayoendelea ya Israel huko Gaza.

Mwanasiasa wa Uswidi Bungeni Ulaya Alipofanya Maandamano ya Ishara ya Ukimya Kuhusu Gaza + Picha

Mwanasiasa wa Uswidi Bungeni Ulaya Alipofanya Maandamano ya Ishara ya Ukimya Kuhusu Gaza + Picha

Katika hotuba yake, Al‑Sahlani alifunika mdomo wake kwa mkono mmoja na kuinua mkono mwingine uliopakwa rangi nyekundu, akiashiria damu na mateso. 

Alibaki kimya kwa sehemu kubwa ya muda wake wa kuongea, kabla ya kusema: 

"There are no more words to speak about what’s going on in Gaza

(Hamna maneno mengine ya kusema kuhusu kilichoko - kinachoendelea- Gaza), na kuongeza kuwa Haki za Binadamu zina rangi ya ngozi - “human rights have a skin colour, and the darker you are the less human rights you have”.

Mwanasiasa wa Uswidi Bungeni Ulaya Alipofanya Maandamano ya Ishara ya Ukimya Kuhusu Gaza + Picha

Al‑Sahlani pia alitaja ujumbe huu maarufu: “Silence is compliance”, akisisitiza kwamba ukimya wa Ulaya unachangia hali hiyo.

Mwanasiasa wa Uswidi Bungeni Ulaya Alipofanya Maandamano ya Ishara ya Ukimya Kuhusu Gaza + Picha

Your Comment

You are replying to: .
captcha