Mufti aliwatambua na kuwapongeza wanahabari hao kwa moyo wao wa kujitolea, akisema juhudi zao ni hazina kubwa kwa Uislamu na jamii kwa ujumla. Alisema uandishi wa habari za Kiislamu unahitaji nidhamu, maarifa, na uaminifu, na hivyo kuwataka waendelee kujifunza na kushirikiana kwa ajili ya mustakabali mwema wa Umma wa Kiislamu.

2 Agosti 2025 - 17:25

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Dar es Salaam – Katika kikao maalum na wanahabari wanaoandika na kusambaza habari za Kiislamu, Mheshimiwa Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir, ametoa wito wa kutumia lugha ya hekima na ulezi katika kazi zao, akisisitiza umuhimu wa kuandika na kusambaza habari sahihi za Kiislamu pasina kupotosha.

Mufti alisisitiza kuwa ni wajibu kwa waandishi wa Kiislamu kutoa taarifa zenye ukweli na uadilifu, hasa kuhusu shughuli za taasisi za Kiislamu na viongozi wake, bila upendeleo wala ubaguzi.

Mufti Apongeza Waandishi wa Habari za Kiislamu kwa Ujitoleaji Wao - Awausia kusambaza Habari za Kiislamu kwa Busara na Ukweli + Picha

Aidha, alieleza kwamba BAKWATA ni Taasisi ya Waislamu wote nchini, na kuwataka waandishi wa habari kuitambua kama chombo chao pia, ambacho kinahitaji kushirikiana nao kwa karibu kwa ajili ya kueneza elimu sahihi na mafundisho ya dini.

Mufti aliwatambua na kuwapongeza wanahabari hao kwa moyo wao wa kujitolea, akisema juhudi zao ni hazina kubwa kwa Uislamu na jamii kwa ujumla. Alisema uandishi wa habari za Kiislamu unahitaji nidhamu, maarifa, na uaminifu, na hivyo kuwataka waendelee kujifunza na kushirikiana kwa ajili ya mustakabali mwema wa Umma wa Kiislamu.

Mufti Apongeza Waandishi wa Habari za Kiislamu kwa Ujitoleaji Wao - Awausia kusambaza Habari za Kiislamu kwa Busara na Ukweli + Picha

Your Comment

You are replying to: .
captcha