Kambi hii iliambatana na maonesho ya Taasisi mbalimbali zilizotambulisha huduma na mafanikio yao, zikiwemo Taasisi ya Kimataifa ya Al-Mustafa (sa) na Mashirika mengine ya maendeleo na kidini.
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Huduma maalum za uchunguzi na matibabu ya macho zilitolewa (kuanzia tarehe: 01/08/2025 - 03/08/2025) kwa Wananchi chini ya uangalizi wa Madaktari Bingwa wa Macho, kwa uratibu wa Jumuiya ya Khoja Shia Ithnaashari ya Dar es Salaam, kwa kushirikiana na wataalamu wa afya kutoka ndani na nje ya nchi.
Kambi hii iliambatana na maonesho ya Taasisi mbalimbali zilizotambulisha huduma na mafanikio yao, zikiwemo Taasisi ya Kimataifa ya Al-Mustafa (sa) na Mashirika mengine ya maendeleo na kidini.
Wageni kutoka Taasisi za Kishia na zisizo za Kishia hapa nchini walihudhuria pia, na kuonesha mshikamano wao katika utoaji wa huduma za kijamii.
Tukio hili limekuwa jukwaa mwafaka la kuimarisha ushirikiano katika sekta ya afya, elimu, na mahusiano kati ya Taasisi za Kidini na Kijamii.
Your Comment