Shule ya Imam Zaynul Aabidin (A.S) imekuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu yenye mchanganyiko wa mafunzo ya dini na maarifa ya kisasa, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya vijana wa Kiislamu kuikabili dunia ya leo kwa maarifa na imani.

7 Agosti 2025 - 12:00

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-, Leo tarehe 7 Agosti 2025 – Darasa maalum la kompyuta limefanyika leo katika Shule ya Imam Zaynul Aabidin (A.S) Nchini Burundi, likiwashirikisha Wanafunzi wa shule hiyo chini ya Usimamizi wa Jamiat Al-Mustafa (s).

Darasa hilo, lililoendeshwa na Ustadh Salim, lilifanyika katika mazingira ya utulivu, na lililenga kuwapatia wanafunzi ujuzi wa msingi kuhusu matumizi ya kompyuta na teknolojia ya kisasa. 

Darasa la Kompyuta lafanyika katika Shule ya Imam Zainul-Abidina (as) Nchini Burundi - Chini ya Usimamizi wa Jamiat Al-Mustafa (s) +Picha

Miongoni mwa mada zilizofundishwa ni utumiaji wa mfumo wa uendeshaji, Programu za Ofisi (Office) kama vile Microsoft Word na Excel, pamoja na utangulizi wa matumizi ya intaneti.

Wanafunzi walionyesha hamasa kubwa katika kujifunza, huku wakisisitiza kuwa maarifa hayo ni muhimu katika mazingira ya sasa ya kidijitali. 

Mwalimu Salim alieleza kuwa madarasa haya yataendelea kufanyika kwa awamu, ili kuhakikisha kila mwanafunzi anapata uelewa wa kutosha.

Darasa la Kompyuta lafanyika katika Shule ya Imam Zainul-Abidina (as) Nchini Burundi - Chini ya Usimamizi wa Jamiat Al-Mustafa (s) +Picha

Shule ya Imam Zaynul Aabidin (A.S) imekuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu yenye mchanganyiko wa mafunzo ya dini na maarifa ya kisasa, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya vijana wa Kiislamu kuikabili dunia ya leo kwa maarifa na imani.

Your Comment

You are replying to: .
captcha