Tunaomba kwa unyenyekevu kwa yeyote atakayeguswa na tukio hili la kusikitisha, achangie kadiri ya alivyoneemeshwa na Allah ili kusaidia watoto hawa ambao wamepoteza sio tu makazi yao, bali pia wenzao waliokuwa nao katika kituo hicho.
Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Leo, tarehe 7 Agosti 2025, Samahat Sheikh Swahibu Shabani, Mudir wa Madrasat Darul-Huda, Tabora, akiambatana na msafara wake, amefanya ziara ya kiutu na Ubinadamu katika Makazi ya Watoto Yatima ya Igambilo, yaliyokumbwa na janga la moto hivi karibuni, na kusababisha vifo vya Watoto Yatima Watano (5) na uharibifu mkubwa wa mali katika Kituo hicho.
Katika ziara hii ya kugusa na kutia faraja nyoyo za walionusurika, msafara huo umefikisha mchango wa mifuko 6 ya saruji (simenti) kwa ajili ya kusaidia ujenzi mpya wa kituo hicho.
Ombi Maalum kwa Wenye Kuguswa:
Tunaomba kwa unyenyekevu kwa yeyote atakayeguswa na tukio hili la kusikitisha, achangie kadiri ya alivyoneemeshwa na Allah ili kusaidia watoto hawa ambao wamepoteza sio tu makazi yao, bali pia wenzao waliokuwa nao katika kituo hicho.
Mwenyezi Mungu awalipe wahisani wote, na azilaze roho za marehemu mahali pema Peponi.
Your Comment