Sheikh Mtulya: "Ni wajibu wa kila Muislamu kujihadhari na vitendo vyote vinavyosababisha Shirki na kuiepuka kwa kauli na vitendo, ili kulinda usafi wa imani na utiifu kwa Mwenyezi Mungu Mmoja".
Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) - ABNA- Leo hii tarehe 15 -08-2025, Sala ya Ijumaa imeswaliwa katika Muswalla wa Jamiat al-Mustafa (s) Jijini Dar es Salaam. Khatibu wa Sala ya Ijumaa, Sheikh Mtulya, alitoa khutba yenye mada ya Shirki na Aina Zake, akieleza maana ya Shirki, madhara yake, na namna inavyopingana na misingi ya Tauhidi.
Katika maelezo yake, Sheikh Mtulya alisisitiza wajibu wa kila Muislamu kujihadhari na vitendo vyote vinavyosababisha Shirki na kuiepuka kwa kauli na vitendo, ili kulinda usafi wa imani na utiifu kwa Mwenyezi Mungu Mmoja
Your Comment