Majalisi hizi pia zimekuwa fursa ya kuonesha mshikamano wa Waislamu wa Tanzania na ulimwengu mzima katika kuhuisha kumbukumbu ya Arubaini ya Imam Hussein (a.s), tukio linalojulikana kwa kuwakutanisha mamilioni ya waumini katika mji wa Karbala kila mwaka.
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Kwa baraka za Mwenyezi Mungu (s.w.t), Waumini wa Kishia nchini Tanzania wameendelea na Majalisi za Arubaini ya Imam Hussein (a.s) katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Arusha. Majalisi hizi ni sehemu ya kumbukumbu ya msiba mkubwa wa Karbala, ambapo Mjukuu wa Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w), Imam Hussein (a.s), alisimama kidete dhidi ya dhulma na ufisadi na kutoa muhanga maisha yake pamoja na Ahlul-Bayt wake na wafuasi wake waaminifu kwa ajili ya kuinusuru Haki, Ukweli na Uhakika.
Katika mkusanyiko hii, Muhadhiri Sheikh Maulid Hussein Kundya, alisisitiza kwa Waumini:
1_Umuhimu wa kuendeleza ujumbe wa Karbala: Kusimama na haki na kupinga dhulma.
2_Kudumisha Umoja na Mshikamano wa Waislamu kupitia kumbukumbu ya Ahlul-Bayt (a.s).
3_Kuimarisha maadili ya Kiislamu ya uadilifu, udugu na upendo kwa wanadamu wote.
Majalisi hizi pia zimekuwa fursa ya kuonesha mshikamano wa Waislamu wa Tanzania na ulimwengu mzima katika kuhuisha kumbukumbu ya Arubaini ya Imam Hussein (a.s), tukio linalojulikana kwa kuwakutanisha mamilioni ya waumini katika mji wa Karbala kila mwaka.
Shi'a Ahlul-Bayt (a.s) Tanzania / Mashia Nchini Tanzania:
Jumuiya ya waumini wa Ahlul-Bayt (a.s) nchini Tanzania huandaa Majalisi na shughuli mbalimbali za kidini, hususan katika miezi ya Muharram na Safar, kwa ajili ya kudumisha urithi wa Mtume (s.a.w.w) na kizazi chake kitukufu.
Your Comment