Majlisi hii imehudhuriwa na waumini wengi kutoka maeneo mbalimbali, jambo lililoonesha wazi upendo, uaminifu na utiifu wao kwa mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), Imam Hussein (a.s).
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Kwa idhini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, uongozi wa Hawza ya Imam Ridha (a.s) chini ya usimamizi wa Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Arif Naqvi (Tarehe 15 Agosti 2025 | 1446 Hijiria) uliandaa kwa heshima kubwa maadhimisho ya Arubaini ya Imam Hussein (a.s) katika kituo cha Kisayansi (Kielimu) ya Kiislamu, kilichopo Ikwiriri - Rufiji, Tanzania.
Majlisi hii imehudhuriwa na waumini wengi kutoka maeneo mbalimbali, jambo lililoonesha wazi upendo, uaminifu na utiifu wao kwa mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), Imam Hussein (a.s).
Tukio hili pia limekuwa fursa ya kukumbusha funzo la subira, ushujaa na kusimama imara dhidi ya dhulma kama lilivyojidhihirisha katika tukio la Karbala.
Mhubiri wa maadhimisho haya, Sheikh Hamimu Mgagi, alitoa hotuba yenye maudhui mazito na yenye taathira kubwa kwa waumini.
Katika maelezo yake, alifafanua juu ya Hotuba za Sayyidat Zainab (s.a) na Imam Zaynul Abidin (a.s) walizozitoa mbele ya Muovu Yazid bin Muawia, na kuonesha namna walivyohifadhi heshima, imani na ukweli katika mazingira magumu ya dhulma na huzuni.
Maadhimisho yalipambwa na kusomwa kwa marthiya, mashairi na nauha za maombolezo pamoja na dua maalum kwa ajili ya mshikamano na umoja wa Waislamu.
Uongozi wa Hawza uliwashukuru wote waliohudhuria na wale waliounga mkono programu hii, huku ukisisitiza kwamba Arubaini ni fursa ya kufufua thamani za uadilifu na utafutaji na uhuishaji wa haki ambazo Ahlul-Bayt (a.s) walizisimamia na kusimama kuzitetea.
Your Comment