Bw. Xavery Kapinga, Mtaalamu wa Maabara: "Damu huhitajika zaidi na wakina mama wakati wa kujifungua, waathirika wa ajali, na wagonjwa wa selimundu (sickle cell)".
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Dar -es- Salaam – Tanzania, 17-08-2025 Katika kuadhimisha Arubaini ya Imam Hussein (a.s), Taasisi za kijamii: Beyond Ethnicity Foundation (BEF) na Nyota Foundation (NF), kwa udhamini wa Care Aid Africa Foundation, ziliandaa tukio la uchangiaji damu katika maeneo ya Chekechea, Mikwambe, Temeke - Dar es Salaam.
Wananchi wengi walijitokeza kwa moyo wa huruma kuchangia damu kwa ajili ya wagonjwa wenye uhitaji Hospitalini. Zoezi hilo lilitekelezwa na wataalamu wa afya kutoka Hospitali ya Vijibweni, Kigamboni, kwa kushirikiana na Kitengo cha Damu Salama.
Bw. Xavery Kapinga, Mtaalamu wa Maabara, alieleza kuwa wachangiaji damu wanatakiwa kuwa na sifa kama vile: Umri wa Miaka 18–68, afya njema na uzito usiopungua kilo 50, na wasiathirike na magonjwa sugu au ya kuambukiza.
Alibainisha kuwa damu huhitajika zaidi na wakina mama wakati wa kujifungua, waathirika wa ajali, na wagonjwa wa selimundu (sickle cell).
Tukio hili limeonyesha mshikamano wa kijamii na kiimani, likiwa ni sehemu ya kuhuisha kumbukumbu ya kujitolea na ubinadamu wa Imam Hussein (a.s).
Your Comment