Picha hizi katika tukio hili, zinaonyesha uhusiano wa karibu kati ya uongozi wa kimataifa wa Kiislamu na wanazuoni wa mataifa mbalimbali, hasa wakati huu wa ibada ya Arubaini inayokusanya mamilioni ya mahujaji (mazuwwari) kutoka pande zote za dunia.

18 Agosti 2025 - 12:21

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s) –ABNA– Wakati wa kipindi cha Arubaini ya Imam Hussein (a.s), Ayatollah Reza Ramezani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Kimataifa wa Ahlul-Bayt (a.s), akiwa katika Mji Mtukufu wa Karbala, alikutana na kufanya mazungumzo na kundi la wanazuoni, wanafikra, na wanaharakati wa kidini na kitamaduni kutoka nchi mbalimbali duniani.

Mikutano hii, iliyofanyika kwa nyakati tofauti, ilikuwa fursa ya kujadili masuala muhimu ya umma wa Kiislamu, hali ya Waislamu katika maeneo mbalimbali ya dunia, na umuhimu wa kuimarisha mshikamano kati ya wapenzi wa Ahlul-Bayt (a.s).

Ripoti hii ya picha inaonyesha uhusiano wa karibu kati ya uongozi wa kimataifa wa Kiislamu na wanazuoni wa mataifa mbalimbali, hasa wakati huu wa ibada ya Arubaini inayokusanya mamilioni ya mahujaji (mazuwwari) kutoka pande zote za dunia.

Your Comment

You are replying to: .
captcha