Sheikh H.Jalala alisema: “Nimemsoma Mtume Muhammad (s.a.w.w), tabia na maadili yake. Mtume alikuwa mtu mwenye uwezo wa kuishi na kila mtu katika jamii. Sheikh Iddi Yasin alijipamba kwa tabia hii ya Mtume, na jamii imemtambua hivyo. Huenda kwa sababu ya kufanana huku, Mwenyezi Mungu amemchukua katika siku hizi za kumbukumbu ya kifo cha Mtume (s.a.w.w).”

23 Agosti 2025 - 09:27

Mazishi ya Sheikh Iddi Yasin yafanyika Temeke sambamba na Maadhimisho ya Kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w) +Picha

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-: Dar es Salaam - Tanzania, Leo hii (jana Ijumaa), Waumini wa Madhehebu mbalimbali pamoja na ndugu, jamaa na marafiki walijumuika katika viwanja vya Hawza ya Bilal Muslim - Temeke, Dar es Salaam, kushiriki katika mazishi ya Sheikh Iddi Yasin, aliyekuwa mwalimu, mpenzi na mfuasi wa Ahlul-Bayt (a.s). Tukio hili lilienda sambamba na Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Mazishi ya Sheikh Iddi Yasin yafanyika Temeke sambamba na Maadhimisho ya Kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w) +Picha

Mazishi haya yalihudhuriwa na Waislamu wa Shia na Sunni, wakitoa taswira ya mshikamano na upendo wa Kiislamu, huku wote wakisindikiza mwili wa marehemu ambaye alijulikana kama kipenzi cha kila mtu kutokana na tabia na mwenendo wake mwema.

Katika marasimu hayo, Sheikh Hemed Jalala, Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Ithna Ashari Tanzania (T.I.C), alitoa khutba fupi na yenye mafunzo muhimu. Katika hotuba yake, aligusia kumbukumbu ya kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w) na kifo cha Sheikh Iddi Yasin, akieleza kuwa kuna mafunzo ya kipekee katika kuondoka kwake siku hizi tukufu.

Mazishi ya Sheikh Iddi Yasin yafanyika Temeke sambamba na Maadhimisho ya Kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w) +Picha

Sheikh H.Jalala alisema:

“Nimemsoma Mtume Muhammad (s.a.w.w), tabia na maadili yake. Mtume alikuwa mtu mwenye uwezo wa kuishi na kila mtu katika jamii. Sheikh Iddi Yasin alijipamba kwa tabia hii ya Mtume, na jamii imemtambua hivyo. Huenda kwa sababu ya kufanana huku, Mwenyezi Mungu amemchukua katika siku hizi za kumbukumbu ya kifo cha Mtume (s.a.w.w).”

Mazishi ya Sheikh Iddi Yasin yafanyika Temeke sambamba na Maadhimisho ya Kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w) +Picha

Mazishi haya yameacha funzo kubwa la mshikamano wa Kiislamu na ukumbusho wa umuhimu wa kuiga maisha na tabia za Mtume Muhammad (s.a.w.w) katika maisha ya kila siku.

Mazishi ya Sheikh Iddi Yasin yafanyika Temeke sambamba na Maadhimisho ya Kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w) +Picha

Your Comment

You are replying to: .
captcha