Katika Majlisi hiyo, walihudhuria wazungumzaji mahiri akiwemo Dkt. Rayhani Yasin, Dkt. Swaleh Maulid, pamoja na wasomi wengine wa Sayansi ya Kiislamu.
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Leo hii tarehe 24 -08- 2025, Waumini, Wafuasi na Wapenzi wa Mtume Muhammad (saww) na Aali zake Muhammad (a.s), wakiwa katika hali ya majonzi na huzuni kubwa kwa kuondokewa na Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w), wahudhuri kwa wingi katika Majlisi ya maombolezo ya Kifo cha Mtume (s.a.w.w) iliyofanyika katika Markazi ya Imam Ridha (a.s) – Ikwiriri, Wilaya ya Rufiji, Mkoa wa Pwani, chini ya uongozi wa Sayyid Arif Naqvi.
Katika Majlisi hiyo, walihudhuria wazungumzaji mahiri akiwemo Dkt. Rayhani Yasin, Dkt. Swaleh Maulid, pamoja na wasomi wengine wa Sayansi ya Kiislamu.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu awape wote umri mrefu na afya njema, ili waendelee kuwa walinganiaji wa haki, warithi wa mafundisho ya Mtume (s.a.w.w), na wathamini wa urithi wa Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w), InshaAllah.
Your Comment