Hotuba mbalimbali zilitolewa zikibainisha nafasi ya Imam Reza (a.s) katika kudumisha elimu na uongozi wa kiroho katika Uislamu.
25 Agosti 2025 - 09:26
News ID: 1719969
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Dar-es-Salaam - Tanzania - Majlisi maalumu ya kumbukizi ya kifo cha Imam Ali bin Musa ar-Ridha (a.s) imefanyika katika mitaa ya Kariakoo, jijini Dar-es-Salaam, ambapo waumini wengi walikusanyika kwa mapenzi ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) na Ahlul-Bayt wake watoharifu (a.s).
Mahudhurio
Hafla hii ya maombolezo imehudhuriwa na:
- Waumini kutoka sehemu mbalimbali za jiji la Dar-es-Salaam.
- Wapenzi na wafuasi wa Ahlul-Bayt (a.s).
- Wanafunzi wa Chuo cha Kisayansi cha Jamiat Al-Mustafa (s), kilichopo Mbezi Beach – Dar-es-Salaam.
Shughuli zilizofanyika
Katika Majlisi hiyo kulisomwa:
- Aya za Qur’an Tukufu.
- Nauha na Marsia za maombolezo,
- Hotuba zilizobainisha nafasi ya Imam Reza (a.s) katika kudumisha elimu na uongozi wa kiroho katika Uislamu.
Umuhimu
Majlisi kama hizi zinaendelea kudumisha:
- Mapenzi ya Waislamu kwa Ahlul-Bayt (a.s),
- Kuimarisha mshikamano wa kijamii na kiroho,
- Kuelimisha vizazi vipya kuhusu historia ya Maimamu watoharifu (a.s).
Your Comment