Katika tukio hilo, waumini wengi walihudhuria kwa wingi kushiriki kwenye maombolezo hayo ya kidini yaliyosheheni qiraa ya Qur’an, majlisi za huzuni na hotuba mbalimbali.
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Kagera – Muleba, Wafuasi wa Ahlul-Bayt (a.s) mkoani Kagera wamefanya Majlisi ya kuhuisha kumbukumbu ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) katika viwanja vya Masjid Ahlul-Bayt (a.s) iliyopo Katobago, wilayani Muleba.
Katika tukio hilo, waumini wengi walihudhuria kwa wingi kushiriki kwenye maombolezo hayo ya kidini yaliyosheheni qiraa ya Qur’an, majlisi za huzuni na hotuba mbalimbali.
Miongoni mwa mada zilizotiliwa mkazo katika hotuba hizo ni mafunzo ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) pamoja na wasia wake wa mwisho kwa Umma wa Kiislamu kuhusu kushikamana na Qur’an Tukufu na kizazi chake kitoharifu, Ahlul-Bayt (a.s).
Waumini walielezwa kuwa kushikamana na wasia huo ni njia ya kudumisha mwongozo wa Mtume (s.a.w.w) na kuimarisha mshikamano wa Kiislamu.
Your Comment