Mjadala wa darasa hilo ulihusu kuongeza maarifa ya kidini, kujisafisha nafsi na kupata hamasa kutoka kwenye mafunzo ya Kiislamu. Wahadhiri waligusia umuhimu wa manufaa ya wakati wa asubuhi (saharuki) katika kujenga hali ya kiroho na kuimarisha mwenendo wa kimaadili wa wanafunzi.
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Leo hii Jumanne, Tarehe 26 Agosti 2025 - Darsa la asubuhi lililojulikana kama “Darsa la Subhi ya Kiroho” limefanyika katika Chuo cha Kisayansi cha Jamiat Al-Mustafa (s) - Mbezi Beach, Jijini Dar-es-salaam, likiongozwa na wahadhiri mashuhuri, Dkt. Saleh Maulid na Dkt. Ali Maamari anayetoka nchini Iran.
Mjadala wa darasa hilo ulihusu kuongeza maarifa ya kidini, kujisafisha nafsi na kupata hamasa kutoka kwenye mafunzo ya Kiislamu. Wahadhiri waligusia umuhimu wa manufaa ya wakati wa asubuhi (saharuki) katika kujenga hali ya kiroho na kuimarisha mwenendo wa kimaadili wa wanafunzi.
Kwa kupitia masomo hayo, washiriki walihimizwa kujenga nidhamu ya maisha ya kiroho na kuendeleza uhusiano wao na Mwenyezi Mungu kupitia mazingatio ya kila siku.
Your Comment