Kikao hiki kimeacha athari chanya kwa washiriki, kwani kilikuwa ni kianzio cha siku kilichojaa baraka, elimu, na msukumo wa kiroho.
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Asubuhi ya leo, Tarehe 27 Agosti 2025, Jumatano - Wanafunzi wa Taasisi waliungana katika kikao maalumu cha kimaadili na kiroho kilichoongozwa na Sheikh Ghawthi. Lengo kuu la darasa hili lilikuwa ni kuwajengea washiriki mtazamo sahihi juu ya umuhimu wa kuanza siku kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu, kujenga nidhamu ya nafsi, na kutumia ipasavyo muda wa asubuhi kwa ibada na maendeleo ya kimaadili.
Katika mawaidha yake, Sheikh Ghawthi alisisitiza kuwa:
Saa za mwanzo wa siku zina nafasi kubwa katika kuimarisha ukaribu wa mja na Mola wake.
Kujitathmini na kujisahihisha ni nguzo muhimu ya kujenga nafsi bora.
Kuzingatia ibada za asubuhi kunampa Mwanafunzi nguvu za kiroho na kisaikolojia kwa ajili ya majukumu ya siku nzima.
Wanafunzi walioshiriki walionekana na hamu kubwa, huku wakitoa ushirikiano wa karibu kwa maswali, majadiliano na kutafakari kwa pamoja. Hali hii ilileta mazingira ya utulivu, nuru na mshikamano wa kiimani, jambo lililowafanya wengi kutamani kuendeleza utamaduni huu kila siku.
Kwa ujumla, kikao hiki kimeacha athari chanya kwa washiriki, kwani kilikuwa ni kianzio cha siku kilichojaa baraka, elimu, na msukumo wa kiroho.
Your Comment