Aidha, alisisitiza juu ya umuhimu wa kinga ya magonjwa kwa kupitia mtindo bora wa maisha, lishe yenye usawa, na ufuatiliaji wa mara kwa mara wa afya

29 Agosti 2025 - 10:32

Jamiat Al-Mustafa (s) - Dar-es-salaam | Kikao cha Kielimu cha Tiba: Dkt. Ali Memari Aendeleza Mafunzo ya Afya Binafsi na Kijamii

Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Leo (Jana -Alhamisi) 28/8/2025 - Darasa la Tiba lilitolewa katika Chuo cha Kisayansi cha Jamiat Al-Mustafa (s), kupitia 
Mwalimu wa Tiba: Dkt. Ali Memari, kutoka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Katika kikao hiki, Dkt. Ali Memari aliendeleza mafunzo yake ya kielimu na kitabibu, akilenga kuinua uelewa wa kiafya na kuimarisha maarifa ya vitendo kwa wanafunzi katika nyanja za afya binafsi na kijamii.

Aidha, alisisitiza juu ya umuhimu wa kinga ya magonjwa kwa kupitia mtindo bora wa maisha, lishe yenye usawa, na ufuatiliaji wa mara kwa mara wa afya. Pia, alitoa mifano ya changamoto za kiafya zinazokumba jamii na njia za kitaalamu za kukabiliana nazo, ili wanafunzi waweze kutumia maarifa haya si tu kwa manufaa yao binafsi, bali pia kwa kutoa huduma na ushauri bora ndani ya jamii.

Jamiat Al-Mustafa (s) - Dar-es-salaam | Kikao cha Kielimu cha Tiba: Dkt. Ali Memari Aendeleza Mafunzo ya Afya Binafsi na Kijamii

Your Comment

You are replying to: .
captcha