Ziara hii imelenga kuimarisha hamasa ya kielimu, kuunga mkono juhudi za walimu na wanafunzi, pamoja na kuonyesha sapoti na mshikamano mkubwa wa Uongozi wa Jamiat Al-Mustafa (s) kwa taasisi zake zote za Sayansi ya Kiislamu ndani na nje ya Tanzania.

29 Agosti 2025 - 14:01

Dr. Ali Taqavi: Mabinti wa Kiislamu Wanapaswa Kuwa Nuru Inayong’aa Katika Jamii ya Kitanzania

Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Dar es Salaam, Leo (Ijumaa), Tarehe 29 Agosti 2025 - Rais wa Jamiat Al-Mustafa (s) tawi la Dar es Salaam, Hujjatul Islam wal-Muslimin Dr. Ali Taqavi, leo ametembelea Hawza ya Mabinti ya Hazrat Zainab (sa) iliyopo Kigamboni, Jijini Dar es Salaam, ambapo alikutana na wanafunzi pamoja na walimu wa kituo hicho cha kielimu na kiroho.

Katika hotuba yake, Dr. Taqavi aliwahimiza mabinti wa Kiislamu wanaosoma katika madrasa hiyo kujituma zaidi katika masomo yao ya Sayansi ya Kidini, akisisitiza umuhimu wa uelewa wa kina na ufaulu bora. Pia aliwakumbusha kuwa Sayansi ya Kiislamu ni msingi thabiti wa malezi ya jamii, na kwamba wao, kama mabinti wa Kiislamu, wanapaswa kuwa mabalozi bora wa elimu ya Kiislamu ili baadaye waweze kuwa nuru inayong’aa katika jamii ya Kitanzania.

Dr. Ali Taqavi: Mabinti wa Kiislamu Wanapaswa Kuwa Nuru Inayong’aa Katika Jamii ya Kitanzania

Ziara hii imelenga kuimarisha hamasa ya kielimu, kuunga mkono juhudi za walimu na wanafunzi, pamoja na kuonyesha sapoti na mshikamano mkubwa wa Uongozi wa Jamiat Al-Mustafa (s) kwa taasisi zake zote za Sayansi ya Kiislamu ndani na nje ya Tanzania.

Dr. Ali Taqavi: Mabinti wa Kiislamu Wanapaswa Kuwa Nuru Inayong’aa Katika Jamii ya Kitanzania

Your Comment

You are replying to: .
captcha