Uwepo wa JMAT katika tukio hili muhimu uliashiria mshikamano na Ushirikiano wa karibu kati ya taasisi za dini na serikali katika kujenga umoja, mshikikano na maendeleo ya kitaifa.

30 Agosti 2025 - 11:19

Askofu Dkt. Israel Laizer Aongoza Ujumbe wa JMAT Katika Mapokezi ya Mkuu Mpya wa Mkoa wa Arusha, Mheshimiwa Amosi Makala + Picha

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Arusha, TanzaniaJumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT), imeshiriki katika mapokezi rasmi ya Mkuu Mpya wa Mkoa wa Arusha, Mheshimiwa Amosi Makala.

Katika hafla hiyo iliyoandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, viongozi wa dini na mila walipewa nafasi maalum ya kumuombea dua ya baraka kwa Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa, ili Mwenyezi Mungu amjalie ufanisi na baraka katika utekelezaji wa majukumu yake mapya ya uongozi.

Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT) iliakisi uwakilishi bora kupitia viongozi wake wa taifa na mkoa wa Arusha, wakiongozwa na Katibu Mkuu wa JMAT Taifa, Mheshimiwa Askofu Dkt. Israel Maasa Ole Gabriel Laizer.

Askofu Dkt. Israel Laizer Aongoza Ujumbe wa JMAT Katika Mapokezi ya Mkuu Mpya wa Mkoa wa Arusha, Mheshimiwa Amosi Makala + Picha

Uwepo wa JMAT katika tukio hili muhimu uliashiria mshikamano na Ushirikiano wa karibu kati ya taasisi za dini na serikali katika kujenga umoja, mshikikano na maendeleo ya kitaifa.

Mapokezi haya yameibua ari na matumaini mapya ya mshikamano wa kijamii na kidini katika Mkoa wa Arusha, huku yakionesha uthamini mkubwa wa viongozi wa serikali kwa mchango wa viongozi wa dini katika kuimarisha amani, mshikamano na maendeleo ya Wananchi.

Your Comment

You are replying to: .
captcha