Kwa ujumla, kisomo cha leo kimetoa taswira ya mshikamano wa kijamii, na kuonyesha namna dini, siasa na jamii zinavyoweza kushirikiana kwa amani na mshikamano katika kuhifadhi maadili na utu wa mwanadamu.

31 Agosti 2025 - 21:27

Waislamu Dar es Salaam Waungana Kumuombea Marehemu Bi. Amina Sungura katika Kisomo cha Siku 40

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Leo hii, tarehe 30 Agosti, 2025- Waislamu wa Jiji la Dar es Salaam, wakiongozwa na ndugu, jamaa, marafiki na wakazi wa Mtaa wa Sukuma, Kariakoo, wameungana katika Kisomo cha siku 40 kuomboleza na kuenzi maisha ya Marehemu Bi. Amina Sungura.

Waislamu Dar es Salaam Waungana Kumuombea Marehemu Bi. Amina Sungura katika Kisomo cha Siku 40

Hafla hiyo ya maombi na kisomo imefanyika kwa heshima kubwa na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali mashuhuri, akiwemo Mheshimiwa Mussa Zungu Mussa, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ilala, na Haji Manara, Mkurugenzi wa Manara TV na Mgombea wa Udiwani, ambao walijiunga na waombolezaji wengine katika kusoma dua na kuonyesha mshikamano na familia ya marehemu.

Kisomo hicho kilijumuisha mawaidha ya Kiislamu, dua maalum kwa ajili ya Marehemu, na kumbukumbu ya mchango wake katika familia na jamii, ambapo watu wengi walieleza jinsi alivyokuwa mkarimu, mpenda watu, na mwenye mchango wa dhati kwa majirani na wapendwa wake.

Waislamu Dar es Salaam Waungana Kumuombea Marehemu Bi. Amina Sungura katika Kisomo cha Siku 40

Ushiriki wa viongozi wa kisiasa katika tukio hilo umeonekana kama ishara ya mshikamano wa kweli baina ya viongozi na wananchi, sambamba na kudhihirisha utamaduni wa Watanzania wa kushikamana katika nyakati za huzuni na furaha. Tukio hili limeongeza hisia ya kuimarika kwa mahusiano ya kijamii, kisiasa na kidini ndani ya jamii ya Kariakoo na Mkoa wa Dar es Salaam kwa ujumla.

Waislamu Dar es Salaam Waungana Kumuombea Marehemu Bi. Amina Sungura katika Kisomo cha Siku 40

Kwa ujumla, kisomo cha leo kimetoa taswira ya mshikamano wa kijamii, na kuonyesha namna dini, siasa na jamii zinavyoweza kushirikiana kwa amani na mshikamano katika kuhifadhi maadili na utu wa mwanadamu.

Waislamu Dar es Salaam Waungana Kumuombea Marehemu Bi. Amina Sungura katika Kisomo cha Siku 40

Your Comment

You are replying to: .
captcha