Majlisi hii ilikuwa ni fursa muhimu ya kuonyesha mapenzi ya dhati kwa mjukuu kipenzi wa Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w) na kuhuisha upendo wetu kwa Ahlul-Bayt (as).
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-Leo, Jumanne tarehe 1 Septemba 2025, Hawza ya Mabinti ya Hazrat Zainab (sa) iliyoko Kigamboni, Dar es Salaam, imefanya Majlisi Maalum ya Maombolezo kwa heshima ya kumbukumbu ya kuuawa shahidi kwa Imam Hassan Al-Askari (A.S).
Katika kikao hiki kilichojaa heshima na unyenyekevu kwa ajili ya mjumbe mtukufu wa Ahlul-Bayt (a.s), mzungumzaji mkuu alikuwa ni Samahat Sheikh Swaleh Maulid, ambaye alitoa khutuba yenye mawaidha ya thamani juu ya maisha, elimu, na msimamo wa Imam Al-Askari (a.s) katika kudumisha Uislamu wa kweli.
Wahudhuriaji wa kikao hiki walikuwa ni wanafunzi wote wa Hawza pamoja na waumini mbalimbali kutoka maeneo ya jirani waliokuja kushiriki na kupata sharafu ya kuwepo katika maombolezo haya.
Majlisi hii ilikuwa ni fursa muhimu ya kuonyesha mapenzi ya dhati kwa mjukuu kipenzi wa Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w) na kuhuisha upendo wetu kwa Ahlul-Bayt (as).
Kushiriki kwa kila mmoja wenu ni mchango muhimu katika kuhuisha mapokeo ya Kiislamu na kudumisha heshima ya familia ya Mtume Mtukufu (s.a.w.w).
Your Comment