Imam Al-Askari (a.s): Mwanga wa Elimu na Subira Akumbukwa katika Kituo cha Al_Kawthar, Kigoma +Picha
Kwa heshima ya kumbukumbu ya kuuawa shahidi kwa Imam Hasan Al-Askari (a.s), mmoja wa Maimamu wa Nyumba ya Mtume (s.a.w.w), Majlisi Maalum ya Maombolezo imefanyika katika Kituo cha Al-Kawthar (a.s) kilichopo Kigoma, nchini Tanzania, mnamo tarehe 8 Rabi’ul-Awwal 1447 Hijria.
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-Leo hii, Tarehe: 1 Septemba, 2025, Sawa na tarehe 8 Rabi’ul-Awwal 1447H, imekuwa ni Siku ya Huzuni kwa Wafuasi wa Mtume Muhammad na Aali zake Muhammad (Amani iwe juu yao) amba Majlisi adhimu ya Kumuomboleza Imam Hassan Al-Askari (a.s) imefanyika kwa Hamasa kubwa katika Kituo cha Kidini cha Al-Kawthar - Kigoma, Tanzania.
Kwa heshima ya kumbukumbu ya kuuawa shahidi kwa Imam Hasan Al-Askari (a.s), mmoja wa Maimamu wa Nyumba ya Mtume (s.a.w.w), Majlisi Maalum ya Maombolezo imefanyika katika Kituo cha Al-Kawthar (a.s) kilichopo Kigoma, nchini Tanzania, mnamo tarehe 8 Rabi’ul-Awwal 1447 Hijria.
Katika majlisi hii, waumini wamekusanyika kwa pamoja kwa ajili ya:
- Kumuomboleza kwa huzuni Shahidi huyu Mtukufu wa Ahlul-Bayt (a.s).
- Kusoma mawaidha juu ya maisha, elimu, na juhudi za Imam katika kuhifadhi Uislamu wa kweli.
- Kufanya dua na matam ya huzuni kuonyesha mapenzi na utiifu kwa kizazi kitakatifu cha Mtume (s.a.w.w).
"A’dhamallāhu ujūrana wa ujūrakum" – Mwenyezi Mungu atuongezee sisi na nyinyi malipo adhimu kwa msiba huu mkubwa.
Imam Hasan Al-Askari (a.s) ni Nani?
- Ni Imam wa 11 katika mlolongo wa Maimamu wa Ahlul-Bayt (a.s)
- Alizaliwa mwaka 232 Hijria na akafa shahidi mwaka 260 Hijria akiwa na umri wa miaka 28.
- Alishi kipindi kigumu cha ukandamizaji wa utawala wa Abbasiyya lakini alihifadhi elimu ya Ahlul-Bayt na kuwaandaa wafuasi kwa kipindi cha Ghayba ya mwanawe, Imam Mahdi (a.t.f.s).
Imam Hasan Al-Askari (a.s) alisimama imara katika kueneza elimu, kujenga imani ya kweli miongoni mwa Waislamu, na kupambana na upotoshaji wa dini katika mazingira ya ukandamizaji mkubwa wa kisiasa.
Tanbihi:
Majlisi kama hizi ni sehemu muhimu ya kuenzi historia ya Uislamu na kuonyesha uaminifu wetu kwa njia ya Ahlul-Bayt (a.s). Zinaimarisha mapenzi kwa watu wa nyumba ya Mtume na kuendeleza urithi wao katika nyoyo za waumini.
Your Comment