Hafla hii ilidhihirisha mshikamano wa Ummah wa Kiislamu na mapenzi ya kweli kwa Mtume Muhammad (saww), huku washiriki wakieleza furaha yao kwa kushiriki tukio hili kubwa la kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Kiongozi wa Rehma
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Korogwe, Tanga - Tanzania, Maelfu ya Waumini wa Kiislamu kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania na nje ya nchi walijumuika kwa pamoja kusherehekea Maulid ya Kitaifa ya Kuzaliwa kwa Mtume Mtukufu Muhammad Al-Mustafa (saww) katika hafla adhimu iliyofanyika mjini Korogwe, mkoa wa Tanga.
Hafla hiyo ya kiroho na kihistoria iliambatana na picha na taswira mbalimbali zilizoonyesha mapokezi makubwa, mshikamano wa waumini, na hali ya furaha iliyojaa mapenzi kwa Mtume wa Ummah na Rehma kwa walimwengu wote.
Katika Maulid hiyo, Waumini walipata fursa ya kusikiliza mawaidha ya dini, qaswida, na hotuba kutoka kwa viongozi wa dini waliogusa nyoyo za wengi kwa ujumbe wa amani, upendo, na kuenzi mafundisho ya Mtume Muhammad (saww).
Hafla hii ilidhihirisha mshikamano wa Ummah wa Kiislamu na mapenzi ya kweli kwa Mtume Muhammad (saww), huku washiriki wakieleza furaha yao kwa kushiriki tukio hili kubwa la kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Kiongozi wa Rehma.
Your Comment