"Upandishaji wa Bendera hii unatufunza kuwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) ametufundisha Amani, Upendo na Kushikamana. Kuishi kwa misingi hiyo kutaiwezesha nchi yetu kuwa ya amani, yenye mshikamano na mapenzi ya kweli kati ya wananchi wake"
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Dar es Salaam – Katika kuadhimisha Maulidi ya Mtume Muhammad (s.a.w.w), tukio la heshima la kupandisha Bendera ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) limefanyika leo katika Msikiti wa Ghadiir, uliopo Kigogo Post, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa shughuli hiyo, Sheikh Jalala alieleza kuwa:
"Upandishaji wa Bendera hii unatufunza kuwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) ametufundisha Amani, Upendo na Kushikamana. Kuishi kwa misingi hiyo kutaiwezesha nchi yetu kuwa ya amani, yenye mshikamano na mapenzi ya kweli kati ya wananchi wake".
Shughuli hiyo imelenga kuwahamasisha waumini na jamii kwa ujumla kuenzi mafunzo ya Mtume (s.a.w.w) kwa vitendo, hasa katika kipindi hiki muhimu cha Wiki ya Umoja wa Kiislamu.
Maulidi rasmi ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) yatafanyika siku ya Jumatano, tarehe 10 Septemba 2025, ambapo waumini na wananchi wote wanakaribishwa kushiriki katika hafla hiyo adhimu ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Rehma kwa walimwengu wote.
Your Comment