Hafla hiyo imekuwa sehemu ya maandalizi muhimu ya kusherehekea siku hii tukufu, ikisisitiza umuhimu wa Qur’an katika maisha ya Waislamu na nafasi ya umoja wa waumini katika kuiadhimisha kwa heshima siku ya kuzaliwa kwa Mtume wa mwisho wa Mwenyezi Mungu.
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-Samahat Sheikh Mohammed Khalaf Zadeh, Qarii mashuhuri wa Qur’an Tukufu kutoka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, amewagusa waumini kwa kisomo chake kizuri cha aya tukufu za Qur’an katika usiku wa leo wa kuamkia hafla ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (rehema na amani zimshukie yeye na Aali zake).
Waumini pamoja na wanafunzi wa Hawza ya Hazrat Zainab (sa) - Kigamboni, Dar-es-salaam, walihudhuria katika hafla fupi ya usiku huo, wakiwa na hamasa kubwa ya kusikiliza maneno matukufu ya Mwenyezi Mungu na kujiandaa kwa sherehe kuu ya Maulidi ya Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Your Comment