Tunawashukuru sana washiriki wote wa tukio hili tukufu. Mwenyezi Mungu awabariki nyote kwa kuonyesha Mapenzi yenu makubwa kwa Mtume Muhammad (Rehma na Amani ziwe juu yake) na Aali zake Muhammad.
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Leo (Jumapili) tarehe 7/9/2025, Chuo cha Kimataifa cha Al-Mustafa Tanzania kimeadhimisha Wiki ya Umoja na kuzaliwa kwa Mtume wetu Kipenzi Muhammad (saww) pamoja na Imam Ja’far Sadiq (as) katika ukumbi wa Al-Mustafa uliopo Kigamboni - Jijini Dar-es-salaam.
Maelfu ya Waislamu kutoka umma mbalimbali walihudhuria tukio hili adhimu.
Sherehe ilianza kwa kisomo cha Qur'an Tukufu, kisha wahadhiri mbalimbali walitoa mihadhara yao.
Dkt. Ali Taqavi, Mkuu wa Chuo cha Al-Mustafa - Tanzania, alitoa hotuba muhimu ya ukaribisho iliyojikita katika umuhimu wa Umoja baina ya Waislamu.
Viongozi wengine waliotoa hotuba ni pamoja na Sheikh Dkt.Abdur Razzaq, Sheikh Dkt.Alhad Musa, Sheikh Ali Ngeruko ambaye ni Naibu Kadhi Mkuu wa Tanzania na Mjumbe wa Baraza la Ulamaa, Sheikh Hemed Jalala ambaye ni Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shi'a Ithna Ashari Tanzania, Mama Shamim Khan, Mwenyekiti wa Juwakita na Waziri Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo wote waligusia historia ya Mtume Mtukufu (saww).
Tunawashukuru sana washiriki wote wa tukio hili tukufu. Mwenyezi Mungu awabariki nyote kwa kuonyesha Mapenzi yenu makubwa kwa Mtume Muhammad (Rehma na Amani ziwe juu yake) na Aali zake Muhammad.
Your Comment