"Mtume Muhammad (saww) ni Kiumbe Bora na Mkamilifu Zaidi wa Mwenyezi Mungu"
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-Siku ya Jumatano, tarehe 10 Septemba 2025, hafla fupi na ya kiroho iliandaliwa katika Jumuiya ya Al-Mustafa (S.A.W.W), mjini Dar es Salaam, Tanzania, kwa ajili ya kuadhimisha siku tukufu ya kuzaliwa kwa Mtume wa Uislamu, Muhammad Mustafa (S.A.W.W).
Mtoa mada rasmi katika hafla hiyo alikuwa Sheikh Muhammad Munito, ambaye alitoa hotuba yenye mada ya:
"Kiumbe Bora na Mkamilifu Zaidi wa Mwenyezi Mungu".
Katika mawaidha yake, alieleza daraja ya kipekee ya Mtume (S.A.W.W) katika uumbaji wa Mwenyezi Mungu, akitaja sifa zake za kipekee katika tabia, ujumbe na maisha yake.
Sherehe hiyo ilihudhuriwa na wanafunzi wa dini, walimu na wapenzi wa Mtume Muhammad na Aali zake Muhammad (Amani ya Allah iwe juu yao), na ilihitimishwa kwa dua na Salawat kwa Mtume Muhammad na Ahlul-Bayt wake (A.S).
Your Comment