Muendelezo wa Mapenzi kwa Mtume (saww) Hafla ya Maulid Kigogo ni moja ya mfululizo wa matukio yanayoandaliwa kila mwaka kwa lengo la kuimarisha mapenzi ya Waislamu kwa Mtume Muhammad (saww), sambamba na kuhimiza utekelezaji wa mafundisho yake katika maisha ya kila siku.
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Dar es Salaam, 10 Septemba 2025 – Maelfu ya waumini kutoka ndani na nje ya Mkoa wa Dar es Salaam wamejitokeza kwa wingi katika viwanja vya Pipo, kushiriki katika Kilele cha Maulid Kigogo 2025, hafla adhimu ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtukufu Mtume Muhammad (saww).
Hafla hii tukufu imeongozwa na Maulana Sheikh Hemed Jalala Mwakindenge, ambaye alisisitiza juu ya umuhimu wa kuiga maisha na mafunzo ya Mtume (saww) katika kujenga jamii yenye maadili, huruma, na mshikamano.
Wageni Maalum Waliopata Sharafu ya Kuhudhuria katika Hafla hii adhimu
Katika kuonesha mapenzi yao kwa Mtume Muhammad (saww), wageni mashuhuri kutoka ndani na nje ya nchi walihudhuria tukio hili, akiwemo:
- Hujjatul Islam Dr. Ali Taqavi, Rais wa Jamiat al-Mustafa (s) – Tanzania
- Dr. Maarifi, Mkurugenzi wa Kitengo cha Utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
- Masheikh mbalimbali kutoka jiji la Dar es Salaam na mikoa mingine ya Tanzania, ambao kwa pamoja walitoa khutba, nasaha, na mawaidha ya kuhamasisha umoja wa Kiislamu na ufuasi wa kweli kwa Mtume wa Rehema (saww).
Muendelezo wa Mapenzi kwa Mtume (saww)
Hafla ya Maulid Kigogo ni moja ya mfululizo wa matukio yanayoandaliwa kila mwaka kwa lengo la kuimarisha mapenzi ya Waislamu kwa Mtume Muhammad (saww), sambamba na kuhimiza utekelezaji wa mafundisho yake katika maisha ya kila siku.
Wahudhuriaji walipata fursa ya kusikiliza qaswida, burdah, khutuba za kielimu, pamoja na dua maalum zilizoambatana na shangwe na bashasha za kumkumbuka Mtume wa mwisho (saww).
Your Comment