Kilichoongeza nuru na baraka zaidi katika sherehe hii ya Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (s a.w.w) ni ushiriki wa ndugu zetu Waislamu wa Madhehebu ya Kisunni, hususan wafuasi wa Madhehebu ya Shafi‘i, ambao walihudhuria kwa heshima kubwa na kushirikiana katika hafla hii ya umoja na mapenzi kwa Mtume wa Uislamu wote.
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Leo hii Tarehe: 13/9/2025 - Sherehe tukufu ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume wa Uislamu, Mtume Muhammad al-Mustafa (s.a.w.w.), imefanyika kwa adhama kubwa katika mji wa Bujumbura - Burundi. Tukio hili limehudhuriwa na idadi kubwa ya waumini wa Madhehebu ya Kishia kutoka maeneo mbalimbali ya jiji hilo na vitongoji vyake.
Kilichoongeza nuru na baraka zaidi katika sherehe hii ni ushiriki wa ndugu zetu Waislamu wa Madhehebu ya Kisunni, hususan wafuasi wa madhehebu ya Shafi‘i, ambao walihudhuria kwa heshima kubwa na kushirikiana katika hafla hii ya umoja na mapenzi kwa Mtume wa Uislamu wote.
Hotuba zilizotolewa katika sherehe hii zilibeba ujumbe muhimu wa kidini na kijamii, zikisisitiza kauli mbiu kuu:
“Mtume Muhammad (s.a.w.w.) ni alama ya umoja wa Kiislamu.”
Wahadhiri walifafanua nafasi ya Mtume katika kuunganisha nyoyo za Waislamu, kuvunja mipaka ya tofauti ndogondogo za madhehebu, na kujenga jamii yenye mshikamano, mshikikano na mshikamani.
Sherehe hii yenye baraka ilifanyika katika uwanja wa Msikiti Mkuu wa Burundi (Grand Mosque of Burundi), ambapo nyimbo za kaswida, usomaji wa Qur’ani, na dua za pamoja zilifanyika, na hali ya furaha na mshikamano ikatawala.
Kwa ujumla, tukio hili liliakisi sura ya kweli ya maadhimisho ya Maulidi ya Mtume (s.a.w.w.) kama nyenzo ya kuimarisha mapenzi, mshikikano, na mshikamano kati ya Waislamu wa pande zote, bila kujali tofauti za madhehebu.
Your Comment