Dr.Taqavi, aliwapongeza walimu na wasimamizi kwa juhudi zao za kuhakikisha malengo ya taasisi yanatekelezwa ipasavyo.
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-Rais wa Jamiat al-Mustafa (s) - Tanzania, Dr. Ali Taqavi, amefanya kikao maalumu na walimu wa taasisi hiyo kwa ajili ya kujadili masuala muhimu ya kielimu, kijamii, kitamaduni za Kiislamu, pamoja na maendeleo ya chuo kwa ujumla.
Katika kikao hicho, Mkuu wa Jamiat Al-Mustafa (s) alieleza kuridhishwa kwake na mwenendo mzuri wa kazi zinazotekelezwa katika sekta mbalimbali chini ya usimamizi thabiti na wa kuridhisha.
Aidha, aliwapongeza walimu na wasimamizi kwa juhudi zao za kuhakikisha malengo ya taasisi yanatekelezwa ipasavyo.
Dr. Taqavi aliwahimiza wote kuongeza bidii na kujituma zaidi katika kazi zao, akisisitiza kuwa thamani kubwa zaidi katika kazi ni kujitolea kwa moyo safi na kuhakikisha ubora wa hali ya juu katika kila jukumu. Alibainisha kuwa kazi yoyote ikifanywa kwa nia safi na kiwango bora, hutoa matokeo chanya yenye manufaa ya kudumu kwa sasa na vizazi vijavyo.
Your Comment