Wanafunzi wanafundishwa kutambua nafasi ya Qur’an kama chanzo cha uongofu, utulivu wa moyo, hekima ya maamuzi, na msaada wa kukabiliana na changamoto za maisha.
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Madrasat ya Mabanati ya Hazrat Zainab (sa) Iliyopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam - Tanzania imepiga hatua kubwa katika darsa zake za Qur’an Tukufu chini ya uongozi na Usimamizi wa Rais wa Jamiat al-Mustafa (s) - Tanzania Dr.Ali Taqavi, hususan katika Darsa za Qur'an zinazoendeshwa na Mwalimu wa Qur'an Sheikh Muhammad Ja’far. Wanafunzi, mabinti wa Kiislamu, wanajitahidi kwa bidii katika kujifunza Sayansi za Qur’an, kuzihifadhi Aya zake, na kuzihuisha ndani ya nyoyo na maisha yao ya kila siku.
Darsa hizi zinalenga kuwajenga kuwa kizazi bora cha mabinti wa Kiislamu walio imara katika msingi thabiti wa kiroho na kielimu, kwa mtazamo kuwa Qur’an ni mwongozo wa maisha na uhai wetu.
Pia, wanafunzi wanafundishwa kutambua nafasi ya Qur’an kama chanzo cha uongofu, utulivu wa moyo, hekima ya maamuzi, na msaada wa kukabiliana na changamoto za maisha.
Zaidi ya yote, Qur’an inafundishwa kama mshirika na muombezi wa Muislamu Siku ya Kiyama, huku ikimulika njia yake duniani na kumuinua katika ngazi za juu Peponi.
Your Comment