Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - Leo hii tarehe 25-09-2025 ; Darasa la Qur’ani Tukufu limeendelea katika Chuo Cha Al-Mustafa - Dar-es-salaam - Tanzania chini ya usimamizi wa Walimuajiri na Wapenzi wa Qur'an Tukufu: Sheikh Muhammad Jaafar na Qaari Sheikh Hamis Mpili Kikao hiki cha Kielimu kiliandaliwa kwa lengo la kuinua uelewa wa Qur’an, kuboresha usomaji sahihi kwa kutumia kanuni za Tajwidi na kuwahimiza wanafunzi kufuata mafundisho ya Qur’an Tukufu. Qaari Sheikh Hamis, kwa usomaji wake mzuri wa Qur’an, aliunda mazingira ya kiroho yenye mvuto wa pekee, na Sheikh Muhammad Jaafar alieleza kwa undani maana na ujumbe wa Aya husika za Qur'an Tukufu.

25 Septemba 2025 - 23:51

Darasa la Qur’an Tukufu Lawa Kivutio cha Kiroho na Kielimu kwa Wanafunzi wa Jamiat al-Mustafa (s) Dar-es-Salaam +Picha

Your Comment

You are replying to: .
captcha