Abbas Ali Mwinyi alifariki dunia jana mjini Unguja, na maziko yake yamefanyika leo katika makaburi ya Bweleo, yakiwa ni sehemu ya heshima za mwisho kwa marehemu. Familia, ndugu, jamaa na marafiki walijumuika kumuenzi na kumuombea katika safari yake ya mwisho.

26 Septemba 2025 - 20:03

Viongozi Wa Kitaifa Wamuenzi 'Abbas Mwinyi' Kwa Kushiriki Mazishi na Maziko Yake Zanzibar +Picha

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira ameungana na viongozi wakuu wa kitaifa akiwemo Mgombea mwenza wa Urais, Dkt. Emmanuel Nchimbi, katika kushiriki mazishi naaziko ya Abbas Ali Mwinyi, mtoto wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Hayati Ali Hassan Mwinyi, yaliyofanyika leo katika kijiji cha Bweleo, Zanzibar.

Viongozi Wa Kitaifa Wamuenzi 'Abbas Mwinyi' Kwa Kushiriki Mazishi na Maziko Yake Zanzibar +Picha

Viongozi Wa Kitaifa Wamuenzi 'Abbas Mwinyi' Kwa Kushiriki Mazishi na Maziko Yake Zanzibar +Picha

Katika tukio hilo la majonzi, Wasira alitoa salamu za pole kwa Mgombea Urais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ambaye pia ni ndugu wa marehemu Abbas Mwinyi.

Viongozi Wa Kitaifa Wamuenzi 'Abbas Mwinyi' Kwa Kushiriki Mazishi na Maziko Yake Zanzibar +Picha

Mazishi hayo yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa na chama, wakiwemo viongozi wa serikali, wanasiasa na wananchi, waliokusanyika kuomboleza pamoja na familia ya marehemu.

Viongozi Wa Kitaifa Wamuenzi 'Abbas Mwinyi' Kwa Kushiriki Mazishi na Maziko Yake Zanzibar +Picha

Abbas Ali Mwinyi alifariki dunia jana mjini Unguja, na maziko yake yamefanyika leo katika makaburi ya Bweleo, yakiwa ni sehemu ya heshima za mwisho kwa marehemu. Familia, ndugu, jamaa na marafiki walijumuika kumuenzi na kumuombea katika safari yake ya mwisho.

Viongozi Wa Kitaifa Wamuenzi 'Abbas Mwinyi' Kwa Kushiriki Mazishi na Maziko Yake Zanzibar +Picha

Your Comment

You are replying to: .
captcha