Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kidini na serikali, wakiongozwa na mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mheshimiwa Saidi Mtanda. Aidha, mgeni maalumu katika shughuli hiyo alikuwa Naibu Kadhi na Mjumbe wa Baraza la Ulamaa BAKWATA, Sheikh Ally Ngeruko.
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shi'a Ithna Ashari Tanzania (T.I.C), Maulana Sheikh Hemed Jalala, amesisitiza kuwa amani na mshikamano wa Waislamu na Watanzania kwa ujumla ni jambo la msingi na la lazima kuimarishwa, hususan katika kipindi hiki tunapoelekea uchaguzi mkuu.
Kauli hiyo aliitoa leo - usiku wa kuamkia tarehe (28-09-2025) katika hafla ya Maulid ya Mkoa wa Mwanza iliyoandaliwa na BAKWATA.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kidini na serikali, wakiongozwa na mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mheshimiwa Saidi Mtanda. Aidha, mgeni maalumu katika shughuli hiyo alikuwa Naibu Kadhi na Mjumbe wa Baraza la Ulamaa BAKWATA, Sheikh Ally Ngeruko.
Kauli mbiu za hafla hiyo zilisisitiza mshikamano na umoja wa kitaifa, zikisisitizwa kwa maneno yafuatayo:
#UmojaNdioMsingiWetu | #UmmaMmoja | #KitabuKimoja | #MtumeMmoja
Your Comment