Sheikh Jalala aliongozana na jopo la viongozi kutoka Dar es Salaam akiwemo Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Ndugu Eng. Issa Ruchwengura, pamoja na viongozi wengine wa TIC. Ushiriki wao ulitilia mkazo mshikamano wa Waislamu nchini na umuhimu wa kuenzi mafunzo ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) kama msingi wa umoja na mshikamano wa kitaifa.

28 Septemba 2025 - 16:57

Maulid ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) Yaunganisha Viongozi wa Dini Mkoani Mwanza | Sheikh H.Jalala Aongoza Ujumbe wa T. I. C Katika Maulid hiyo +Picha

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Tanzania (TIC), Maulana Sheikh Hemedi Jalala Mwakindenge, ameshiriki katika maadhimisho ya Maulid ya Bwana Mtume Muhammad (s.a.w.w) yaliyofanyika Jana tarehe 27 -08-2025 Mkoani Mwanza.

Sherehe hizo za Maulid, ambazo zimekusanya mamia ya waumini na wageni waalikwa, zilihudhuriwa pia na viongozi mbalimbali wa kidini wakiongozwa na Sheikh wa Mkoa wa Mwanza wa BAKWATA, Sheikh Kabeke, ambaye ndiye mwenyeji wa hafla hiyo.

Maulid ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) Yaunganisha Viongozi wa Dini Mkoani Mwanza | Sheikh H.Jalala Aongoza Ujumbe wa T. I. C Katika Maulid hiyo +Picha

Sheikh Jalala aliongozana na jopo la viongozi kutoka Dar es Salaam akiwemo Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Ndugu Eng. Issa Ruchwengura, pamoja na viongozi wengine wa TIC. Ushiriki wao ulitilia mkazo mshikamano wa Waislamu nchini na umuhimu wa kuenzi mafunzo ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) kama msingi wa umoja na mshikamano wa kitaifa.

Maulid ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) Yaunganisha Viongozi wa Dini Mkoani Mwanza | Sheikh H.Jalala Aongoza Ujumbe wa T. I. C Katika Maulid hiyo +Picha

Kauli mbiu zilizotumika katika hafla hiyo zilisisitiza mshikamano wa Waislamu na heshima na upendo kwa Mtume Mtukufu (saww), zikisomeka kama ifuatavyo:
#MtumeMmoja | #UmmaMmoja | #KitabuKimoja | #MuhammadMtumewaAmani | #MadrasaAhlulBayt | #IgogoMwanza

Your Comment

You are replying to: .
captcha